Ijumaa 3 Oktoba 2025 - 20:27
Kulinda Muqawama na damu za Mashahidi ni amana iliyopo shingoni mwetu

Hawza / Hospitali ya Darul-Hikma huko Baalbek imeadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah, Sayyid Hashim Safiuddīn, pamoja na mashahidi watatu.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hospitali ya Darul-Hikma huko Baalbek iliadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa shahada ya makatibu wakuu wawili wa zamani wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddīn, pamoja na mashahidi watatu kutoka miongoni mwa wafanyakazi wake: Muhammad Atwi, Husayn al-Nimr na Muhammad Wahbi.

Katika hafla hiyo walihudhuria Ali al-Muqdad, Mjumbe wa Bunge la Lebanon na mwanachama wa kundi la wabunge wa “Uaminifu kwa Muqawama”, Jamal al-Taqsh, Mkurugenzi wa hospitali na mbunge wa zamani, pamoja na watendaji wa hospitali, madaktari, wauguzi, wataalamu wa kiufundi, na viongozi wa kijamii na kiafya.

Al-Muqdad: “Shahidi Nasrallah hajaondoka miongoni mwetu, bali yupo hai katika nyoyo na dhamiri zetu.”

Katika hotuba yake, al-Muqdad, ambaye ni mwakilishi wa bunge, alitoa pongezi kutokana na huduma kubwa zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wananchi wa eneo hilo. Alisisitiza nafasi muhimu ya mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiuddīn katika kuisaidia hospitali hiyo kwa malezi ya kimaanawi na kimaada, jambo lililowezesha hospitali kuwahudumia na kutibu majeraha ya watu wema na waaminifu wa eneo hilo.

Alisema: “Shahidi Sayyid Nasrallah hajaondoka miongoni mwetu; yupo hai katika nyoyo, akili na dhamiri zetu. Mtu huyu wa kipekee alikuwa na ataendelea kuwa kiongozi mwenye kuleta msukumo si kwetu sisi pekee, bali kwa watu wote wapenda uhuru ulimwenguni kote.”

Mjumbe huyo wa kundi la “Uaminifu kwa Muqawama” alisisitiza: “Tunafanya ahadi na Mwenyezi Mungu kama tulivyofanya na mashahidi wote kwamba Muqawama huu utahifadhiwa, utakua na kuenea katika roho, akili na ardhi yetu. Damu za mashahidi ni amana shingoni mwetu, na tutailinda. Hili ni jukumu la kimaadili, kibinadamu na kimungu.”

Aliongeza kuwa yeyote atakayepuuza jukumu hili atakuwa amesaliti ubinadamu na kutoa fursa kwa nguvu za shari na giza kueneza dhulma, uharibifu na kiburi cha nguvu za ubeberu katika eneo na dunia nzima.

Al-Taqsh: “Wosia mkuu wa Shahidi Nasrallah ulikuwa ni kulinda Muqawama.”

Kwa upande wake, al-Taqsh alibainisha kuwa sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Darul-Hikma mwezi Februari 1999 ilifanyika kwa uungaji mkono wa Katibu Mkuu wa Hizbullah na Shahidi wa Ummah, Sayyid Hassan Nasrallah. Alisema walichukua usimamizi wa hospitali hiyo kutoka kwa Shahidi Sayyid Hashim Safiuddīn mnamo Juni 22, 2022, baada ya kuwa chini ya uangalizi wa Taasisi ya Kiislamu ya Hospitali.

Aliongeza kuwa: “Kwa hiyo, tuna jukumu kubwa la kuhifadhi amana hii kwa njia inayostahili viongozi wawili hawa waliokuwa mashahidi wabeba haki na waliopanda daraja la shahada wakiwa thabiti mbele ya dhulma. Tunawasilisha rambirambi zetu kwa Sahibu-l-Asr wal-Zamān (aj) kutokana na shahada yao na ya kundi la wafanyakazi wa hospitali waliopanda shahada katika njia ya Quds, kulinda nchi na watu wetu dhidi ya nguvu za shari na uvamizi.”

Al-Taqsh alihitimisha kwa kusema: “Tunaahidi kuwa tutatekeleza wasia wa mashahidi wetu wema kwa kuwahudumia watu, na kufuata mfano wa bwana wa mashahidi wa Muqawama, aliyesema: ‘Tutakuhudumieni kwa nafsi zetu zote.’ Wosia mkuu wake ulikuwa ni kulinda Muqawama, na sisi tumeazimia kutekeleza ahadi hiyo.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha